Joel 2:2-7


2 asiku ya giza na huzuni,
siku ya mawingu na utusitusi.
Kama mapambazuko yasambaavyo
toka upande huu wa milima
hata upande mwingine
jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja.
Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamani
wala halitakuwepo tena kamwe
kwa vizazi vijavyo.

3 bMbele yao moto unateketeza,
nyuma yao miali ya moto
inawaka kwa nguvu.
Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni,
nyuma yao ni jangwa lisilofaa:
hakuna kitu kinachowaepuka.

4 Wanaonekana kama farasi;
wanakwenda mbio
kama askari wapanda farasi.

5 cWanatoa sauti kama magari ya vita,
wanaporukaruka juu ya vilele vya milima,
kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua,
kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita.


6 dWanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu;
kila uso unabadilika rangi.

7 eWanashambulia kama wapiganaji wa vita;
wanapanda kuta kama askari.
Wote wanatembea katika safu,
hawapotoshi safu zao.
Copyright information for SwhKC